Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Majid Takht-Ravanchi amesema kuwa, kurejea Marekani katika makubaliano ya nyuklia na kufungamana kwake na ahdi zake kwa mujibu wa makubaliano hayo ya JCPOA siyo jambo linalohitajia mazungumzo.
Ameeleza kuwa, vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vinapaswa kuwa viwe vimeondolewa katika kipindi cha miezi mitatu ijayo ambapo ni baada ya hatua hiyo ndipo Tehran nayo itarerea katika ahadi zake.
Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameashiria hatua zilizochukuliwa na Iran baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kkueleza kwamba, hatua hizo zimetekelezwa kwa mujibu wa makubaliano hayo na hazipaswi kushadidisha mvutano.
Takht-Ravanchi amesisitiza kuwa, Iran haina haja ya kufanya mazungumzo kuhusiana na suala la kurejea Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA au kufungamana taifa hili na ahadi zake kwa mujibu wa makubaliano hayo.
Aidha mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichoitishwa hivi karibuni kwa ajili ya kuchunguza athari mbaya za kiusalama za mabadiliko ya hali ya hewa kwamba, vikwazo vya kiuchumi vya upande mmoja ni moja ya vizuizi vikuu vinavyokwamisha juhudi za kukabiliana ipasavyo na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi, hivyo lazima viondolewe.
342/